SINA MAMA KUNILEAMama angu simuoni, naambiwa kakimbia
Sina furaha moyoni, mama nilimzoea
Nimebaki ukiwani, ninalia na dunia
Kinda ningali mtini, sina mama kunilea
Mama nilikosa nini, mwanao kunikimbia
Umenitupia nani, mwingine wa kunilea
Nimebaki na huzuni, sina wa kunidekea
Kinda ningali mtini, sina mama kunilea
Mimi na baba nyumbani, wenyewe twajipikia
Baba anachanja kuni, nami nachochea
Hukumbukia zamani, mama ninakulilia
Kinda ningali mtini, sina mama kunilea
Sheikh Amri Abeid Kaluta Sheria za Kutunga Mashairi EALB
Emotions are the greatest enemy of rational arguments