Ndugu zanguni! Sasa kwa vile tumekuwa na wanachama wengi amabao baadhi yao hawasemi Kukuyu, nafikiri wakati umewadia wa kuanza kuchangia mada za Kiswahili. Basi mijadala ya Kiswahili izuke!
Emotions are the greatest enemy of rational arguments
Posts: 3133 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005
Wakanyugui na Beste, Nawashukuru sana kwa kuniunga mkono. Inaonekana ni wakati mzuri kutumia lugha yetu ya Taifa zaidi. Hivi si kumaanisha lugha zetu ni duni. Lakini nafikiri ni vizuri kutia juhudi kuimarisha Kiswahili chetu ili kujenga utamaduni wa Kikenya.
Tuunganeni mikono Kukiimarisha Kiswahili.
Emotions are the greatest enemy of rational arguments
Posts: 3133 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005
hamna lugha yeyote ya mtu mweusi iloyo duni, zote tajiri kuzidia mno. lakini kimombo/kizungu ni lugha duni.
tukumbuke nusu kiswahili ni lugha ya kibantu na kikiyu ni lugha ya kibantu. jambo hili linatufanya ndungu moja.
This message has been edited. Last edited by: Beste,
'kajikatia kanga ya moto ya kifua iliyokwisha fukizwa. Mugongoni kanda za kanchiri zinaonekana zimesaki kwenye misirimbi ya nyama zake za mbega. Mkono unaopuna uso wake kwa shada la kitambaa ulikuwa umeshughulika kuiweka sawa podari.'
Hiyo swahili ya Said A Mohamed kwa kitabu chake Utengano kina nipiga chenga nani atanifafanulia.
Maisha ni ujaliwavyo si utakavyo
Posts: 971 | Location: Gongo la Mboto | Registered: 08 March 2008
Muhuthia, Nahitaji muktadha wa usemi huo. Hebu nambie ukurasa wa kitabu ulichonukuu maneno hayo ili nijaribu kuyafasiri. Kabla sijaondoka, je wahitaji tafsiri ya moja kwa moja au fasiri ya kifungu chenyewe kwa jumla?
Emotions are the greatest enemy of rational arguments
Posts: 3133 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005
Kitabu ni Utengano ukurasa wa kwanza. Ana elezea vile ule binti alikuwa akijirebesha, na kujupodoza lakini yale maneno mapya kwangu kama kanchari, misirimbi, fukizwa.
Naomba radhi hapo awali nilinukuru ki makosa neno 'mbega' sio lakini bega. Kwa ile hali ya kuchanganyikiwa nili changanya maneno tena mno.
Maisha ni ujaliwavyo si utakavyo
Posts: 971 | Location: Gongo la Mboto | Registered: 08 March 2008
Muhuthia, Nimeangalia kamusi sasa hivi na maoini yangu ndiyo haya. Nadhani istilahi ni kanchiri na wala sio kanchari. Maana ya kanchiri ni brassiere. Labda kanchari ni neno lile lile kwa lahaja tofauti
Sipati neno misirimbi katika kamusi, lakini fukizwa ni kitenzi fuka likiwa katika hali ya kutendeshwa. Neno fuka lina maana ya kutoa moshi au mvuke. Katika muktadha huu, tutachukia kitenzi hiki katika hali ya kutendeshea yaani 'fukiza' kwa maana ya 'spray perfunme' P
Emotions are the greatest enemy of rational arguments
Posts: 3133 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005