"Ithe wa Nyambura na Wambui" Platinum Member

|
NWB, Mimi pia natoa shukrani kwa msimamizi kwa kuanzisha baraza hii ili tuweze kubadilishana mawazo. Ni vizuri kujuvunia lugha yetu ya taifa. Nilikuwa nimresafiri kwa siku chache zilizopita ndipo sikuweza kushirikiana nanyi, lakini nimerudi kiotani mwangu. Nitaleta mambo nikishapumzika. Wasalaam.
Emotions are the greatest enemy of rational arguments
|
| |
| Posts: 3133 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005 |  
IP
|
|
"Ithe wa Muthoni na Jayson" Platinum Member
|
Hata mimi nitasema machache kuhusu uzinduzi huu wa baraza hili la Kiswahili nitakalotuwezesha kubadilishana mawazo tukitumia hii lugha tuipendao, lugha ya taifa letu. Nawashukuru wanaohusika na mtandao huu kwa kutupa nafasi ya kuwasabahi na kuwajulia hali wenzetu walio kila upande wa dunia hii kupitia njia hii. Muendelee na mwenendo huo huo. Jukumu liliopo kwa sisi sasa ni kuhakikisha ya kwamba tunaitumia njia hii kwa manufaa yetu na ya ndugu na dada zetu. Mola awalinde na kuwabariki. Wa Wakuru
"mûthuri aikarîire njûng'wa onaga kuraya kûrî kîhîî kîhaicîte mûtî"
|
| |
|