Kikuyu.com    KIKUYU.COM    Forums  Hop To Forum Categories  General Discussions  Hop To Forums  Swahili Speakers    TUSAMEHE
Page 1 2 
Go
New
Find
Notify
Tools
Reply
  
-star Rating Rate It!  Login/Join 
"Ithe wa Nyambura"
Platinum Member
Picture of sajini
Posted
Nani ameiona filamu inayoitwa 'Tusamehe'

Hii ni filamu nzuri ambayo imetolewa na Mtanzania anayeeitwa Josiah Kibera. Inasaili maswala ya mapenzi, ndoa, uaminifu, pamoja na kushughulikuia masuala nyeti kama vile 'Ukimwi'

Napendekeza ukiiona mahali uiangalie kwani ni filamu nzuri sana. Tena, ni vizuri kumwuunga mkono Mwafrika mwenzetu, hata kama Watanzania hawana imani nasi Wakenya.

Mkiweza filamu yake ya "Bongoland" ni nzuri pia. Lakini labda umaarufu wa filamu hizi za Bwana Kibira ni kutumia Lugha ya Kiswahili.


Emotions are the greatest enemy of rational arguments
 
Posts: 2927 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Muthoni na Jayson"
Platinum Member
Posted Hide Post
Ndugu Sajini,
Shukrani mno kwa hayo maelezo kuhusu hio filamu. Ningependa sana kuitazama lakini kuna mushkri kidogo kwa maana sijui niitoe wapi. Je una anwani ambayo mtu anaweza kutumia kutafutia hii filamu?
Alamusiki.


"mûthuri aikarîire njûng'wa onaga kuraya kûrî kîhîî kîhaicîte mûtî"
 
Posts: 2932 | Registered: 04 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Nyambura"
Platinum Member
Picture of sajini
Posted Hide Post
Wa Wakuru,
Nitamwandikia Bwana Kibira barua pepe nimuulize kama kuna DVD au VHF Nairobi. Nitakupaa jibu lake hivi karibuni. Unapongonjea, kujua zaidi kuhusu filamu hii unaweza kuitembelea tuvuti yao hapo chini.

http://www.kibirafilms.com/tusamehe/


Emotions are the greatest enemy of rational arguments
 
Posts: 2927 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Muthoni na Jayson"
Platinum Member
Posted Hide Post
Sajini,
Kwa mara igine natoa shukrani zangu kwa hio tuvuti. Nimeitupia macho na nimeona maelezo waliyo nayo. Walakini mna kitu ningependa kujua zaidi na mahali hii filamu imefanyiwa. Kikazi, ningependa kuinunua kwa manufaa ya maktaba yangu kama itakuwa imefanyiwa nchini Tanzania. Lakini kama imefanyiwa ulaya ma Marekani basi, itanibidi niwafahamishe watafute kutoka upande huo. Mtandao ulionipa haujaelezea kwa kinaga ubaga mle hii filamu imefanyiwa.


"mûthuri aikarîire njûng'wa onaga kuraya kûrî kîhîî kîhaicîte mûtî"
 
Posts: 2932 | Registered: 04 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Nyambura"
Platinum Member
Picture of sajini
Posted Hide Post
Wa wakuru,
Nakuelewa sawasawa. Tatizo ni kwamba jamaa huyu anazitengenezea filamu zake hapa Marekana. Labda suala la hela limemfanya kujaribu bahati yake kama vigogo wa Holywood. Ndoto! ndoto! ndoto! Ijapokuwa mada ya filamu ingalishughulikiwa vilivyo kama ilitengenezwa TZ, ninampa heko kwa kutoa fulamu ambayo imefikia kiwango cha juu.

Licha ya hayo, nafikiri kuna haja kubwa ya kuunda filamu ambazo zinashughulikia masuala tofauti. Ala, Africa si Ukimwi pekee! bado sijaona filamu nzuri ya Kimathi, Mau mau, Patrick Shaw, au kesi ya S.M.Otieno. kama wanaigeria wanaunda filamu zenye mada kama hizo, kwa nini Waswahili wasiweze?


Emotions are the greatest enemy of rational arguments
 
Posts: 2927 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"ithe wa *Dave n vickie*"
Gold Member
Picture of wagithuri***
Posted Hide Post
sajini
Nimetamani sana kuiona filamu hiyo kwa sababu mimi nazipenda sana filamu za mbongo ,nathani nikiitafuta hapa mombasa pengine yaweza kupatikana , shinda kumbwa nikuwa nyingi ya filamu hizi hapa mjini sio original.jambo ambalo linafanya niwasikitikie wasanii wetu.


mbaara ti ucuru!
 
Posts: 1480 | Location: mombasa,{ithukum]KINANGOP {mucii | Registered: 24 March 2006Reply With QuoteReport This Post
"Uga ĩĩtha"
Silver Member
Posted Hide Post
Sajini

Mambo ni hapo!

Kwa kweli, na kubaliana nawe ya kwamba Kenya kuna maswala mengi abayo wasanii wetu wanaweza kuyahifathi kwa kanda za filamu. Najua unamkubuka yule binti Citi -Hasina Kibibi (Mungu aifalinji roho yake). Kipawa alichokua nacho, kingewaelimisha wasanii wetu vilivyo. Walakini, inaonekana wasanii wetu wako bali na hawanjafikia kiwango kama kilichokua na Binti Kibibi. Kwa kweli, wengi wetu walifurahia kile kipindi cha Tausi. Tungetaka kuwaona wasanii wetu wa kituletea filum ata kama ni ya Moi, Wakinyonga, Wacucu $ Wanugu ama Kamlesh.

Sisi kama Kikuyu.com tunawezaje kuwatia moyo hawa wasanii? hilo ndilo swali ningetaka tunjiulize. Itakua muhimu ikia mjadala kama huu umaweza kuleta mafanikio kwa nchi yetu.

Ningeoma muniwiye radhi ikiwa kiswahili changu si sanifu. Ni meka kwa munda bila kutumia kisahili kwa kuandika. Siku hizi mimi naongeya ile kiswahili ya mtaa peke yake, (Ile ya Mama Njeri ).


Cengera Cema
Cema ũgĩ
 
Posts: 87 | Location: Gĩcagi kwao | Registered: 05 June 2006Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Nyambura"
Platinum Member
Picture of sajini
Posted Hide Post
Wagithuri,
Nilikuwa na shughuli nyingi wikendi hadi nikasahau kumwandikia Kibira Barua Pepe, lakini sasa hivi nitafanya hivyo na mara akinipa jawabu, nitakujulisha mara moja.

Riara,
Nakubali kwamba Wakenya wanatakikana waaamke na kujivunia Ukenya wao, Kusema kweli, sikusoma kitabu cha Moi kiklichoandikwa na Morton, lakini sasa nikikiona nitakuisoma. Ukweli ni kwamba enzi ya Moi uhalisia wetu Wakenya. Ni hitoria yetu, na inahitaji kuhifadhiwa.

Filamu ya Rise and Fall of Id Amin ni filamu nzuri, si kwa sababu Amin alikuwa mzuri, lakini kwa sababu inatuonyesha ukurasa muhimu, na wa huzuni wa maisha ya Uganda. Najua Kenya kuna visa vingi vinavyongonjea kutolewa kutoka lindi la giza ili watu wabaini ukweli.

Kuhusu Kibibi, nani asiyelengwa na machozi kuhusu hatima yake? Fikiria msanii kama Wahome Mutahi pia. Ni wakati wa wasanii wa Kenya kuamka na kuliendeleza gurudumu hili. Tukiwa hapo, tusiwasahahu wasanii kama Kina Kihenjo na Wenzake.

"Iganagwo yaari iria yaringa nguyu" Wakikuyu walinena

Kihenjo akituacha leo (hili si ombi langu) tutalia na kumsifu alivyokuwa msanii maarufu. Ni wakati wetu wa kuuondoa unafiki wetu na kuwaunga mkono wasanii iwalio hai, sio waliokufa!


Emotions are the greatest enemy of rational arguments
 
Posts: 2927 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"ithe wa *Dave n vickie*"
Gold Member
Picture of wagithuri***
Posted Hide Post
Njambo ambalo ni bora kufanya kwanza ni kuhakikisha tunanunua DvD ,VCR,VCD,E.T.C ambazo ni original ili wasanii wetu wainuke nakufaindika kwa kazi nzuuri wanaoifanya .

NI vimbaya kutazama na kusikiza filamu ama kaseti ambazo siyo original maana nikama kukamua ngombe kisha uinyime chakura . Inauma sana kuona watu ambao sio wasanii wakifaindika kwa kufanya uragai wa filamu za wasanii.


mbaara ti ucuru!
 
Posts: 1480 | Location: mombasa,{ithukum]KINANGOP {mucii | Registered: 24 March 2006Reply With QuoteReport This Post
"Uga ĩĩtha"
Silver Member
Posted Hide Post
Sajini,

You have just reminded me about the 40 minutes in Entebe, 30 years ago today.


Cengera Cema
Cema ũgĩ
 
Posts: 87 | Location: Gĩcagi kwao | Registered: 05 June 2006Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Nyambura"
Platinum Member
Picture of sajini
Posted Hide Post
Bwana Kibira alijibu barua yangu. Ninayanakili baadhi ya maneno aliyoniandikia hapa chini;

...Kuhusu VHS na DVD za East Africa - Hatuna. Katika Afrika Ya Mashariki tunamtegemea local distributor ambaye yeye ndiye huamua namna yakuisambaza sinema. Mara kwa mara wanatumia VHS na VCD. VCD ni kama DVDila ni utaalamu uliotangulia kabla ya DVD. Sinema kama hii inawekwakwenye VCD mbili

Kwa sasa tuko katika majadiliano na distributo huyo ambaye atapeleka Afrika ya Mashariki nzima. Mipango ikiwiva nitakujulisha....


Na tuzidi kungonjea basi


Emotions are the greatest enemy of rational arguments
 
Posts: 2927 | Location: Neither here nor there | Registered: 03 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Muthoni na Jayson"
Platinum Member
Posted Hide Post
Sajini,
Asante kwa kujitolea kuwasiliana na Bw Kibera. Tutaingojea hio filamu kwa hamu na ghamu.
Jambo la wasanii, nilikuwa naongea na mhusika mmoja mkuu wa kikundi cha wasanii cha "Redykyulass" nilipotaka kujua mahali naweza nikanunua kanda zao original. Hili ndilo lilikuwa jibu lake, "Tembea katika kibanda chochote huko River Road mahali wanauza kanda za muziki na video na ununue huko, sisi hatuna" Sikuamini na nikamuuliza anifafanulie jambo hilo ndiposa akaniambia wao waliamua hawatashindana na hao watu wanaoitwa "pirates". Jambo hilo linikera sana kuona kwamba kuna mtu anayengojea wengine watoe jasho wakijitahidi ili hali yeye anavuna hio jasho yao. Ni hali ya kusitikisha sana.


"mûthuri aikarîire njûng'wa onaga kuraya kûrî kîhîî kîhaicîte mûtî"
 
Posts: 2932 | Registered: 04 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"ithe wa *Dave n vickie*"
Gold Member
Picture of wagithuri***
Posted Hide Post
Ngunjiri,Sajini,Wa kihia,Riara na karuki wa kariuki ,mko wapi ? ni wamiss sana mpaka nikaona sitavumilia tena
Nime miss hoja zenu sana kwa hivyo amkeni.


mbaara ti ucuru!
 
Posts: 1480 | Location: mombasa,{ithukum]KINANGOP {mucii | Registered: 24 March 2006Reply With QuoteReport This Post
"Ithe wa Muthoni na Jayson"
Platinum Member
Posted Hide Post
Wagithuri,
Ningependa kuomba msamaha kwa kutoweka mitamboni hii ya kik.com kwa muda. Nilikuwa na shughuli mbali mbali za kutafuta riziki na kwa hivyo ikanibidi kutoweka kidogo. Masaa nayo yalikuwa yananipa kisogo na inakuwa vigumu sana kuwasiliana na ndugu na dada zangu hapa kwa huu mtandao. Lakini sasa nimerejea na natarajia Mwenyezi akitujaria, tutazidi kubadilishana mawazo kama vile tumefanya hapo awali. Hisia zangu ni kuwa hawa wengine ambao umetaja wako katika hali hio hio na tunawaomber dua na najua watarudi hivi karibuni. Asante sana kwa fikira zako

Wa Wakuru
 
Posts: 2932 | Registered: 04 May 2005Reply With QuoteReport This Post
"ithe wa *Dave n vickie*"
Gold Member
Picture of wagithuri***
Posted Hide Post
Ngunjiri,
nashukuru sana kwa kurundi kwako,ama kwa hakika nilikuwa nimekukosa sana.
nimatumaini yangu kuwa wenzetu wamepata huo ujumbe na zote tutaendelea kuchangia katika kuendeleza mtandau huu.


mbaara ti ucuru!
 
Posts: 1480 | Location: mombasa,{ithukum]KINANGOP {mucii | Registered: 24 March 2006Reply With QuoteReport This Post
  Powered by Social Strata Page 1 2  
 

Kikuyu.com    KIKUYU.COM    Forums  Hop To Forum Categories  General Discussions  Hop To Forums  Swahili Speakers    TUSAMEHE