Kikuyu.com    KIKUYU.COM    Forums  Hop To Forum Categories  General Discussions  Hop To Forums  Swahili Speakers    Baraza la Mawaziri
Go
New
Find
Notify
Tools
Reply
  
Baraza la Mawaziri
 Login/Join
 
Silver Member
Posted
Hivi maajuzi nilikuwa nakumbuka miaka ya themanini wakati wa utawala wa Baba Moi. Redio ilikuwa moja (Sauti ya Kenya). Babu yangu alikuwa msikilizaji maarufu sana wa taarifa za habari. Hata mimi pia akanifanya shabiki wa hizi taarifa.

Basi nalikumbuka kwa umbali baraza la mawaziri la Raisi Moi. Ingawa nilikuwa mtoto, nawakumbuka wafuatao:
1. Makamu wa raisi na pia waziri wa hazina, mwai kibaki (later profesa george saitoti)
2. Katibu wa baraza la mawaziri (somebody arap leting, later prof. mbithi)
3. Waziri wa Kilimo; Elijah Mwangale
4. Waziri wa Elimu; Peter Oloo Aringo
5. Waziri wa Sayansi na Teknologia Tekelezi; Sam Ongeri
6. Waziri wa Habari na Utangazaji; Waruru Kanja
7. Waziri wa Serikazi za Mitaa; William ole Ntimama
8. Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano; Kenneth Matiba
9. Waziri wa Kawi; Nicholas Biwott
10. Waziri wa Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa; Robert Ouko (who was the successor?)
11. Waziri wa Biashara na Viwanda; Dalmas Otieno

Tafadhali nikosoeni na mnikumbushe wafuatao na wengineo:
1. Waziri katika Afisi ya Raisi anayeshughulia Utawala wa Mikoa
2. Waziri wa Utamaduni na Huduma za Jamii
3. Waziri wa Mazingira na Toradhi za Kitaifa
4. Waziri wa Afya (before mwai kibaki)
etc etc.
 
Posts: 34 | Location: Johannesburg | Registered: 11 November 2007Reply With QuoteReport This Post
"ithe wa *Dave n vickie*"
Gold Member
Picture of wagithuri***
Posted Hide Post
AHAA NDUGU YANGU UMENIKUMBUSHA MBALI KWELI PIA MIMI NIKUWA MPENZI WA TAARIFA ZA HABARI NA MATANGAZO YA MPIRA ,


mbaara ti ucuru!
 
Posts: 1485 | Location: mombasa,{ithukum]KINANGOP {mucii | Registered: 24 March 2006Reply With QuoteReport This Post
"Muru wa Njeri"
Silver Member
Picture of Muhuthia
Posted Hide Post
Burundi Nabwera. Maskhalia (finance), GG Kariuki (state)


Maisha ni ujaliwavyo si utakavyo
 
Posts: 971 | Location: Gongo la Mboto | Registered: 08 March 2008Reply With QuoteReport This Post
Silver Member
Posted Hide Post
Pia kulikuwa na: katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Javier Perez De Cuellar!!
 
Posts: 34 | Location: Johannesburg | Registered: 11 November 2007Reply With QuoteReport This Post
Silver Member
Posted Hide Post
Mjuaji.
Vizuri. Hata mimi nazikumbuka siku hizo. Lakini sasa unazungumzia miaka ipi haswa ya themanini? Nashuku unazungumzia baada ya uchaguzi wa 1988

Wakati huo kama sijakosea kulikuwa pia na akina Jackson Angaine (Afisi ya Raisi), Katana Ngala, Sharrif Nassir, Zachary Onyonka, Davidson Kuguru, William Odongo Omamo, James Njiru (Utamaduni), Mmkindia na wengine.

Nadhani Serikali za Mitaa ilikuwa ni Moses Mudavadi.... Sidhani Ntimama alikuwa waziri kabla ya 92.


Cia mburi ni hia!
 
Posts: 25 | Location: Kwa Waithaka (No Nongainuka!) | Registered: 09 April 2006Reply With QuoteReport This Post
Silver Member
Posted Hide Post
Ahaa, naona sasa Wanaruona unawakumbuka vigogo wa siasa miaka ile. Mimi nazungumzia miaka ya themanini mwishoni (late 80's) hadi tisini mwanzoni (early 90's). Wakati ule taariza zote za habari zilikua zaanzia "Mtukufu Rais Daniel Arap Moi, leo ame....". Pia kulikuwa na "maelezo baada ya habari" halafu yanafuatiwa na "matangazo maalum yakifuatiwa na matangazo ya vifo..."
 
Posts: 34 | Location: Johannesburg | Registered: 11 November 2007Reply With QuoteReport This Post
  Powered by Social Strata  
 

Kikuyu.com    KIKUYU.COM    Forums  Hop To Forum Categories  General Discussions  Hop To Forums  Swahili Speakers    Baraza la Mawaziri